Heart Team Africa Foundation

Heart Team Africa Foundation

In the joy of others lies our own

02 Mar

Kikao cha Pili cha Bodi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF)

Kikao cha pili cha Bodi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) kimefanyika 20/2/2026 chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Bodi, Mheshimiwa Mhe. Mussa Azzan Zungu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kikao hicho, Mwenyekiti alipokea taarifa rasmi ya utekelezaji wa shughuli za Foundation kwa mwaka uliopita. Taarifa hiyo ilionesha mafanikio makubwa ambapo takribani watoto 301 wamefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia juhudi za HTAF, kwa gharama ya jumla ya takribani shilingi bilioni 2.7 zilizopatikana kupitia michango na wadau mbalimbali. Aidha, Bodi ilijadili na kupokea mkakati mpya wa kuongeza mapato kwa lengo la kukusanya shilingi bilioni 25. Fedha hizo zitawezesha kupanua wigo wa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto ndani na nje ya nchi, kuimarisha huduma za uchunguzi wa mapema wa magonjwa ya moyo kwa watoto, pamoja na kutoa elimu mashuleni kuhusu afya ya moyo. Vilevile, Foundation imepanga kujenga nyumba maalum ya watoto ijulikanayo kama House of Hope, ambayo itatoa malazi na huduma za msingi kwa watoto wanaopatiwa matibabu pamoja na wale wanaosubiri upasuaji. HTAF inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo na kuimarisha huduma za afya kwa kizazi cha sasa na kijacho.

recent news