Heart Team Africa Foundation

Heart Team Africa Foundation

In the joy of others lies our own

15 Sep

HTAF YAWALETA BAPS KURUDISHA FURAHA YA WATOTO JKCI

Dar es Salaam, 14 September, 2025 – Mkurugenzi wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), Dk. Peter Kisenge, amekabidhiwa rasmi hundi yenye thamani ya shilingi 250,000,000 kutoka kwa viongozi wa BAPS, kama sehemu ya mchango wa taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wasio na uwezo wa kifedha na wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za JKCI jijini Dar es Salaam, likiwa ni utekelezaji wa ahadi ya BAPS iliyotolewa katika harambee iliyohudhuriwa na Heart Team Afrika Foundation (HTAF) tarehe Novemba mwaka 2024, ambapo taasisi hiyo iliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya matibabu ya watoto 1,500 wenye changamoto za magonjwa ya moyo. Dk. Kisenge alionyesha shukrani zake kwa mchango huo mkubwa, akisema kuwa fedha hizo zitawezesha kuongeza huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto walioko kwenye hali ngumu na kusaidia kuboresha maisha yao. “Msaada huu ni msaada muhimu unaotusaidia kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa watoto wenye magonjwa ya moyo. Tunawashukuru wadau wote waliotoa mchango huu,” alisema. Kwa upande wake, viongozi wa BAPS walisema kuwa mchango huu ni sehemu ya jitihada za kuleta mabadiliko chanya kwa watoto walioko JKCI, na kwamba wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wagonjwa wote. Tukio hili linaonesha mshikamano wa taasisi za afya na wadau mbalimbali katika kuhakikisha watoto wenye magonjwa ya moyo wanapata matibabu stahiki na kuishi maisha yenye furaha

recent news