Kikao cha kwanza cha board ya wakurugenzi wa HTAF
Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team Africa Foundation ( HTAF) Mhe. Mussa Azzan Zungu amefungua Rasmi kikao cha kwanza cha bodi ya HTAF ambacho kilihudhuliwa na Bodi ya Wakurugenzi, waasisi wa Taasisi hiyo akiwepo Dr Peter Kisenge Mkurugenzi wa JKCI. Aidha Mwenyekiti wa bodi Aliithibitisha Manejimenti ya Heart Team Team Africa Foundation ikiwa DR Naizihijwa Majani kama Mtendaji Mkuu (HTAF – Chief Executive Officer) Heart Africa Foundation HTAF ni Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na kuratibu matibabu ya magonjwa ya moyo, kutoa elimu kwa wafanyakazi wa afya na jamii kwa ujumla, na kufanya utafiti wa magonjwa ya moyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Aidha Mtendaji Mkuu wa HTAF DR. Naizihijwa Majani alieleza Ukubwa wa tatizo inchini kuwa kila wanapozaliwa Watoto 100 kuna Watoto mmoja au wawili wanazaliwa na tatizo la magonjwa ya moyo kwa Tanzania kutokana na idadi ya watu Takribani Watoto (4,000) wanazaliwa na magonjwa ya moyo kwa mwaka na wengi wao hawana uwezo wa kughalamia matibabu . Mtendaji huyo nkuu aliongeza kwa kusema HTAF imeweza kuwafanyia Upasuaji wa magonjwa ya Watoto 200 kwa kipindi cha janury 2025 mpaka sasa kutokana na michango iliotokana na wadau mbalimbali. Kikao hicho pia kilikuwa na madhumuni ya kujadili utekelezaji wa mipango ya taasisi, kuweka mikakati endelevu ya utekelezaji, na kuboresha huduma zinazotolewa kwa watoto wenye changamoto ya Magonjwa ya Moyo. Bodi iliwashukuru wadau wote waliojitokeza kuchangia fedha na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Watoto wenye uhitaji mkubwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo. Kwa kipekee Bodi ilimshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wa kugharamia matibabu ya Watoto kwa asilimia 70% kwa ajili ya kuwasadia watoto wenye magonjwa ya Moyo. Bodi ya wakurugenzi ya HTAF inapenda kuwaomba wadau na taasisi za serikari na zisizo zakiserikari, wadau mbalimbalikuendelea kushirikiana na HTAF kuendelea kuchangia misaada ya kifedha, vifaa tiba,au huduma ili kuwasaidia Watoto wenye changamoto yay a magonjwa ya moyo waweze kupata matibabu bora na kurejea kwenye maisha yenye Afya.